Key quotes from Shakespeare’s Julius CaesarDownload 39.46 Kb.
Date27.05.2016
Size39.46 Kb.


Key quotes from Shakespeare’s Julius Caesar

(translation by Julius K. Nyerere)

[1]

Act 1, scene 3
Cassius

And why should Caesar be a tyrant then?

Poor man! I know he would not be a wolf,

But that he sees the Romans are but sheep:

He were no lion, were not Romans hinds. Those that with haste will make a mighty fire

Begin it with weak straws: what trash is Rome,

What rubbish and what offal, when it serves

For the base matter to illuminate

So vile a thing as Caesar!


Kitendo cha kwanza, onyesho la tatu
Kasio

Na kwa nini Kaizari awe mdhalimu, sasa? Maskini! Natambua hangekuwa mbwa mwitu Ila kwa kuona kuwa Warumi ni kondoo tu:

Yeye hangekuwa simba Warumi wasingekuwa ni makoo ya paa tu.

Wenye haraka ya moto huanza kwa vijani: Roma umekuwa taka, umekua ni jalala, umekuwa upuuzi, kutumiwa kama nyasi za kukumulikia kitu duni kama Kaizari.
[2]

Act 2, scene 1
Portia

Within the bond of marriage, tell me, Brutus,

Is it expected I should know no secrets

That appertain to you? Am I yourself

But, as it were, in sort or limitation,

To keep with you at meals, comfort your bed,

And talk to you sometimes? Dwell I but in the suburbs

Of your good pleasure? If it be no more,

Portia is Brutus’ harlot, not his wife.


Kitendo cha pili, onyesho la kwanza
Poshia

Nambie, Buruto, hivi kwenye nadhiri za ndoa imesemwa nisijue siri zinazokuhusu? Kumbe mimi ndiyo wewe kama nusunusu tu? Kukaa nawe mezani, kukupozea kitanda, na kuzungumza nawe mara fulani fulani? Hivi niko pembeni tu katika mapenzi yako? Basi kama hivyo ndivyo—hapana kinachozidi Poshia ni kahaba tu siyo mke wa Buruto.[3]

Act 2, scene 2
Caesar

Cowards die many times before their deaths;

The valiant never taste of death but once.


Kitendo cha pili, onyesho la pili
Kaizari

W’oga hufa mara nyingi kabla ya vifo vyao;

Mashujaa hawaonji kifo ila mara moja.


[4]

Act 3, scene 1
Antony [speaking on his own]

And Caesar’s spirit, ranging for revenge,

With Ate [Greek goddess of mischief and ruin] by his side come hot from hell,

Shall in these confines with a monarch’s voice

Cry ‘Havoc,’ and let slip the dogs of war


Kitendo cha tatu, onyesho la kwanza
Antony [anaongea peke yake]

Na roho ya Kaizari ikitafuta kisasi bega kwa bega na Ate mkali toka Jahimu, kwa sauti ya maliki italia kwa nchini, “Shari!” na kuachilia majibwa ya mapigano[5]

Act 3, scene 2
Brutus

If there be any in this assembly, any dear friend of Caesar’s, to him I say, that Brutus’ love to Caesar was no less than his. If then that friend demand why Brutus rose against Caesar, this is my answer: — Not that I loved Caesar less, but that I loved Rome more.
Kitendo cha tatu, onyesho la pili
Buruto

Ikiwa pana mtu ye yote rafiki mpenzi wa Kaizari, kwake nasema kwamba mapenzi ya Buruto kwa Kaizari hayakuwa chini ya mapenzi yake yeye. Ikiwa, basi, rafiki mpenzi huyo atauliza kwa nini Buruto kumshambulia Kaizari, jibu langu ni hili: — Siyo kwa sababu sikumpenda sana Kaizari, bali kwa sababu nilipenda Roma zaidi.
[6]

Act 4, scene 3
Brutus

There is no terror, Cassius, in your threats,

For I am arm’d so strong in honesty

That they pass by me as the idle wind,

Which I respect not.


Kitendo cha nne, onyesho la tatu
Buruto

Vitisho vyako, Kasio, ni vya upuzi kabisa,

kwani ninayo silaha ya kutosha—moyo safi—na nisowaheshimu hunipita kama vumbi.


[7]

Act 4, scene 3
Cassius

You love me not.Brutus

I do not like your faults.Cassius

A friendly eye could never see such faults.Brutus

A flatterer’s would not, though they do appear

As huge as high Olympus.


Kitendo cha nne, onyesho la tatu
Kasio

Hunipendi.Buruto

Sipendi makosa yako.Kasio

Kweli jicho la rafiki kamwe lisingeyaona makosa namna hiyo.Buruto

Jicho lake mnafiki kamwe lisingeyaona

hata kama yangekuwa makubwa kama Olimpo.


[8]

Act 4, scene 3
Brutus

Our legions are brim-full, our cause is ripe:

The enemy increaseth every day;

We, at the height, are ready to decline.

There is a tide in the affairs of men,

Which, taken at the flood, leads on to fortune;

Omitted, all the voyage of their life

Is bound in shallows and in miseries.

On such a full sea are we now afloat;

And we must take the current when it serves,

Or lose our ventures.


Kitendo cha nne, onyesho la tatu
Buruto

...jeshi letu limejaa, nia yetu imeiva:

Na adui kila siku azidi kuongezeka;

Kwa kuwa tu kileleni tutaanza kwenda chini.

Majambo ya binadamu yana kujaa na kupwa,

Yakidakwa yamejaa huongoza ushindini;

yakipuuzwa, safari yote ya maisha yao haiachi maji mafu, na hujaa madhilifu.

Sisi sasa twaelea katika maji makuu;

Twapaswa kuyatumia yangali yakitufaa,

ama sivyo tutakosa yote tuloazimia.[9]

Act 5, scene 1
Brutus

If we do meet again, why, we shall smile;

If not, why then, this parting was well made.


Kitendo cha tano, onyesho la kwanza
Buruto

Endapo tutakutana tutafurahi hakika;

bali tusipokutana kwa heri hii ni sawa.


[10]

Act 5, scene 5
Brutus

Night hangs upon mine eyes; my bones would rest,

That have but labour’d to attain this hour.


Kitendo cha tano, onyesho la tano
Buruto

Sasa usiku wa giza walemea macho yangu; na mifupa yangu nayo,

ilofanya kazi kubwa, kufikia saa hii yataka kupumzika.


[11]

Act 5, scene 5
Antony

This was the noblest Roman of them all:

All the conspirators save only he

Did that they did in envy of great Caesar;

He only, in a general honest thought

And common good to all, made one of them.

His life was gentle, and the elements

So mix’d in him that Nature might stand up

And say to all the world ‘This was a man!’


Kitendo cha tano, onyesho la tano
Antonio

Huyu ndiye alikuwa Mrumi bora wa wote;

Mhaini wale wote, kumwondoa peke yake, walitenda walotenda kwa sababu ya husuda, walivyomhusudia mtukufu Kaizari;

Ila yeye peke yake, kwa nia safi kabisa na kwa faida ya umma, akawa mmoja wao.

Alikuwa mwadilifu mwenye maisha manana;

Na vipaji vilikuwa vimechanganyika kwake,

Miungu wangaliweza kusimama

na kusema, kwa ulimwengu mzima, ‘Huyu alikuwa mtu!’
Share with your friends:
The database is protected by copyright ©www.essaydocs.org 2020
send message

    Main page